Saturday, March 6, 2010

KUNA MAISHA BAADA YA KUFA???

Je kunayo maisha baada ya kifo?



Swali: "Je kunayo maisha baada ya kifo?"

Jibu: Je, kunayo maisha baada ya kifo? Bibilia inatuambia, “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kasha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe… Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena” (Ayubu 14:1-2,14)?

Kama vile Ayubu, karibu sisi sote tumekabiliwa na swala kama hili. Ni jambo gani hasa hutukia kwetu baada ya kufa? Je, ni kukosa kuwepo duniani tu? Je, maisha ni kufa na kufufuka tu ili tujipatie umaarufu tena duniani? Je, watu wote huenda mahali pamoja, au huenda mahali tofauti? Je, kunayo kweli Mbingu na Jehanamu, au ni maneno tu ya kujitungia?

Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia,wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).

Yesu alichukua adhabu aliyostahili kila mmoja wetu na akajitoa maisha yake. Siku tatu baadaye, akathibitisha ushindi wake juu ya mauti kwa kufufuka kutoka kaburini, katika roho na katika mwili. Alibaki katika dunia kwa mda wa siku arubaini na kushuhudiwa na maelfu ya watu kabla ya kupaa nyumbani kwake Mbiguni kwenye uzima wa milele. Warumi 4:25 yasema, “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu,na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.’’

Ufufuo wa Kristo lilikuwa ni jambo lililodhihirika Mtume Paulo aliwapatia watu changamoto kwamba wawaulize wale waliokuwapo wakati jambo hilo likitendeka wahakikishe kama jambo hilo si kweli. Hakuna aliyeweza kushindana juu ya ukweli huo. Ufufuo ndio msingi imara (jiwe la pembeni la) wa imani ya Mkristo; kwasababu Kristo alifufuka katika wafu, sisi pia tunaweza kuwa na imani ya kwamba tutafufuliwa.

Paulo aliwaonya wakristo wa kwanza ambao hawakuyaamini haya: “Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka” (Wakorintho 15:12-13).

Kristo alikuwa pekee wa kwanza kati ya mavuno makuu ya wale watakao inuliwa kutoka kwa wafu. kifo kiliingia duniani kuputia mtu mmoja, Adamu ambaye sisi sote ni wa ukoo wake. lakini wale ambao wamefanywa wana wa Mungu kupitia imani juu ya Yesu Kristo watapewa maisha mapya (Wakorintho wa kwanza 15:20-22). Kama vile Mungu alivyofufua mwili wa Yesu, vivyo hivyo ndivyo miili yetu itakavyofufuliwa Yesu atakaporudi (Wakorintho wa kwanza 6:14).

Ijapokuwa sote tutakuwa tumefufuliwa, hatutaenda sote mbinguni mahali pamoja. Mtu sharti afanye uamuzi wa kuchagua sasa juu ya mahali anapotaka kuenda kwa umilele wake. Bibilia inasema ya kwamba imetupasa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Wale waliotakaswa wataenda kwa uzima wa milele mbinguni, lakini wasioamini watapelekwa kwa hukumu ya milele ama jehanamu (Mathayo 25:46).

Jehanamu, kama vile mbinguni, si mahali patajwapo kwa utisho tu bali ni mahali dhahiri. Hapa ni mahali ambapo wasiohaki watakutana na ghadhabu isiyokoma ya Mungu. Watavumilia mateso ya kihisia, kiakili, na kimwili wakiwa katika akili zao timamu huku wakijihisi kuaibika na kujuta kwa matendo yao maovu.

Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na ziwa la moto, liwakalo na kiberiti amabpo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.

Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele? Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).

Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36). Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya kristo.

Ukitaka kumpokea Yesu kristo kama mwokozi wako, hapa kuna ombi rahisi. Kumbuka kusema ombi hili wala lengine hakutakuokoa kutokana na dhambi zako bali kwa kumwamini kristo pekee. Ombi hili ni njia tu ya kujielezea mbele za mungu juu ya kumwamini kwako na kumshukuru kwa kumtoa njia ya wokovu wako. “Mungu, ninajua ya kwamba nimefanya dhambi na ninapaswa hukumu. Lakini Yesu kristo alichukua adhabu yangu ili kwamba kwa kumwamini yeye nipate msamaha wa dhambi zangu. Ninaghairi dhambi zangu sasa na kuziacha. Ninaweka tumaini langu kwake kwa wokovu wangu. Asante kwa neema yako ya ajabu na msamaha – kipwa cha uzima wa milele!

Amina!”

MUNGU AKUBARIKI!!!!

Friday, March 5, 2010

KAMA WEWE NI MWIMBAKWAYA, ELEWA HISTORIA YA UIMBAJI & MUZIKI.

HISTORIA YA UIMBAJI NA MUZIKI

Uimbaji asili yake ni mbinguni (Eze 28:13-15). Tutakapofika mbinguni tutaendelea kumwimbia Bwana (Ufu 15:2-4; Ufu 5:9-10).


Hapa duniani nyimbo na muziki vilianza zamani sana baada ya kuumbwa kwa Adamu na Hawa "...na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi."(Mwa 4:1-21).

UMUHIMU WA KWAYA KATIKA KANISA

Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja(na kupiga vyombo vya muziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo mpya. Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki (Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet 4:10-11).

Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32). Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Mtu mwenye udhaifu anaweza kusikia nguvu na uzima kwa nyimbo. Daudi alipopiga muziki roho mbaya ilimwacha Sauli (1 Sam 16:23). Tunasoma pia kwamba siku moja Sauli aliingiwa na ghadhabu, chuki na kumwonea Daudi wivu baada ya kusikiliza maneno ya nyimbo (1 Sam 18:6-9).

Nyimbo tunazosikiliza (redioni, katika kanda, nk) kama hazina maneno yenye maadili mazuri, mioyo yetu inaweza kuchafuliwa na kutufanya twende kinyume na mapenzi ya Mungu.

Nyimbo zinavuta nguvu na uwepo wa Mungu (2 Nya 20:21-22; 2 Fal 3:15-16). Paulo na Sila waliomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, hatimaye milango ya gereza ikafunguka (Mdo 16:25-26).

AINA ZA NYIMBO

Nyimbo nyingi zinaangukia katika makundi yafuatayo:

1. Nyimbo za mafundisho/maonyo (Kol 3:16).
2. Nyimbo za faraja
3. Nyimbo za mahubiri (Isa 48:20).
4. Nyimbo za sifa/shukurani/maombi
5. Zipo pia nyimbo za upuzi (Amo 6:5). Mungu hapendi nyimbo za upuzi.


Biblia inatuagiza kuimba "kwa akili" yaani tuimbe huku tukiwa na ufahamu wa nyimbo tunazoimba (Zab 47:6-7; 1 Kor 14:15). Kwa sababu hiyo, wanakwaya wanapaswa pia kujua nyimbo wanazoimba zina maana gani au lengo lake ni nini. Zinahubiri au zinafariji? Zinajenga au zinabomoa? Vinginevyo wanaweza kujikuta wanaimba nyimbo za upuzi au zisizokuwa na maana.

Kama wewe mwenyewe huelewi yale unayoimba, unafikiri wale wanaosikiliza wimbo wako wataelewa? Sio rahisi.

MADA ZA NYIMBO
Wimbo unaweza kuwa na mada (topic) moja au zaidi. Lakini wimbo wenye mada moja ni mzuri zaidi. Kwanini?

1. Wimbo wenye mada moja mara nyingi unaanza kwa utangulizi, baadaye unaelezea mada yenyewe na kisha unatoa hitimisho, kwahiyo ni rahisi kukumbuka ujumbe wa wimbo huo.
2. Unakuwa na ufafanuzi wa kutosha. Beti 3 au 4 zinazungumzia mada moja tu kwa kuifafanua.


Mada ya wimbo inaweza kumlenga mtu mmoja au watu kadhaa:

* waliobatizwa
* mvulana na msichana waliotangazwa kwamba ni wachumba
* maarusi - waliofunga ndoa (Zab 78:63) nk.
* watu ambao hawajaokoka (wanaosikiliza mkutano wa Injili).


"KUMECHISHA"

Neno hilo linatumika kuelezea jinsi mtu alivyovaa mavazi yanayofanana rangi. Mtu anaweza kumwambia rafiki yake: "Aisee, leo umependeza! Umemechisha vizuri sana - kuanzia kichwani hadi miguuni!"

Wakati wa ibada, kwaya inaweza pia "kumechisha" nyimbo zake na mahubiri au tukio la siku hiyo. Kwa mfano, kama mada ya mahubiri ni "Faida za wokovu", kwaya itafute wimbo unaozungumzia wokovu na kuuimba kabla au baada ya mahubiri. Wakati wa mkutano wa Injili, ili "kumechisha," pambio kama hii inafaa kuimbwa" "Akina baba njoni, akina mama, njoni, nanyi vijana njoni, mje muokolewe..."

Wimbo kama huu ufuatao haufai kuimbwa na kwaya wakati mwinjilisti anapokuwa amemaliza kuhubiri mkutano wa Injili: "Sio kila mtu asemaye ameokoka, ataingia mbinguni. Siku ile watasema, 'tulikuwa wahubiri', watakataliwa."

Siku moja mahali fulani kwaya ilikaribishwa iimbe wimbo ili kukamilisha mahubiri ya siku hiyo. Mahubiri yalikuwa mazuri sana lakini bahati mbaya kwaya ile iliimba wimbo "usiomechi" na mahubiri yale: ".. toa kwanza boriti katika jicho lako mwenyewe ndipo utoe kibanzi katika jicho la ndugu yako." Tuimbe kwa akili na pia "tumechishe"!

Ili kwaya iweze kila mara kufaulu kumechisha inahitaji kuwa na nyimbo nyingi, zenye mada mbalimbali. Ni vizuri kila somo katika Biblia liwe na wimbo wake. Yaani ziwepo nyimbo zinazozungumzia wokovu, utakatifu, amri za Mungu, neema, msamaha, ubatizo, ndoa, watoto, utumishi, uinjilisti, maombi nk, nk. Je, kwaya ya Kanisa lako ina nyimbo ngapi? Sulemani alikuwa na nyimbo zaidi ya 1000 (1 Fal 4:29-32).

JINSI YA KUPATA WIMBO/MADA MPYA

Watu wengi wanapenda vitu vipya. Kiatu kipya, gauni jipya, nyumba mpya, vyombo vipya nk. Vivyo hivyo watu wanapenda kusikia nyimbo mpya. Lakini je, ni rahisi kwaya au watunzi wa nyimbo kupata nyimbo mpya kila mara?

Mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kupata nyimbo au mada mpya.

1. Ukisikia sauti ya wimbo (melody) moyoni mwako fanya haraka kuirekodi kwenye kanda (kama una radio cassette na microphone) ili usisahau.
2. Soma Biblia, soma vitabu vya Neno la Mungu. Hudhuria vipindi vya mafundisho. Mada unazozipata zitungie nyimbo. Nyimbo zinazotungwa kwa njia hii ni nzuri kwa sababu zinalingana na Neno la Mungu. Sio rahisi watu kuzikosoa kwamba haziendani na Biblia.
3. Unaposafiri, unapokuwa sokoni nk, sikiliza yale yanayosemwa, tazama yanayofanyika kisha uyatungie nyimbo (za maonyo, za ushauri nk) kulingana na Neno la Mungu.
4. Mwombe Mungu akupe wimbo mpya. Mungu anaweza yote.


Unapokosa maneno ya kuweka katika wimbo sio vizuri kujaziajazia tu maneno au sauti zisizo na maana ili wimbo uimbike!

UPIGAJI WA VYOMBO VYA MUZIKI

Maneno ya nyimbo yanavutia sana yanapoambatana na upigaji mzuri wa vyombo. Biblia inatuagiza tupige kwa ustadi (Zab 33:3). Kila inapowezekana tuwe tayari kujiunga na shule za muziki au kujifunza kwa wale wanaojua ili tuweze kupiga vyombo kwa ustadi. Siku hizi kwenye mtandao kuna masomo mengi ya muziki yanayotolewa bure kuhusu jinsi ya kupiga gitaa, kinanda, jinsi ya kusoma noti za muziki(notation) nk. Tuwe tayari kuyatafuta.

Biblia inasema tusiifuatishe namna ya dunia hii (Rum 12:2a). Hata katika uimbaji na upigaji wa vyombo hatuna haja ya kuifuatisha namna ya dunia hii. Haimpi Mungu utukufu ukisikia mtu anasema: "Kwaya hii imeimba wimbo unaofanana na wimbo wa yule msanii wa muziki kule Marekani (ambaye hajaokoka)." Tunaye Mungu anayeweza kutusaidia kupiga vyombo kwa ustadi. Tumtegemee.

Vyombo vya muziki vinasaidia kubeba ujumbe. Kwahiyo fundi mitambo wa Kwaya ni vizuri ahakikishe kwamba sauti za vyombo hazizidi zile za waimbaji. Vinginevyo watu watasikia tu vyombo na kukosa ujumbe.

MITINDO YA UIMBAJI

Kuna mitindo mbalimbali ya uimbaji. Wengine wanaimba huku wamesimama wima, wengine wanaimba huku wamekaa, na wengine wanaimba huku wakionesha ishara mbalimbali kwa mikono na miguu yao. Mitindo ya uimbaji ni mizuri iwapo tu inasaidia kufikisha ujumbe kwa wahusika. Huduma ya uimbaji sio "show." Hatuimbi ili kuwaonesha wengine kwamba sisi tuna mitindo mizuri ya kuimba. Kwahiyo kwa mfano, kama wimbo una maneno yafuatayo: "Dunia inaangamia. Watu hawamchi Mungu, asubuhi mpaka usiku watu wanakunywa pombe, wanafanya uzinzi, wanapigana. Tuwaombee wasiangamie..." sio vizuri kuuimba wimbo huo kwa mitindo ya shangwe na nyuso zilizojaa furaha. Sio vizuri kwa sababu sio jambo linalofurahisha kuona watu wanaangamia.

UTAKATIFU KATIKA UIMBAJI

Huduma ya uimbaji ni muhimu iendane na maisha ya utakatifu. Mizaha wakati wa mazoezi ya nyimbo haifai. Mizaha ni dhambi (Mit 26:19, 19:29; Zab 1:1).


Kuimba bila utakatifu ni kelele mbele za Bwana (Amo 5:12, 22-23).

Wanakwaya ni walimu. Wanalifundisha Kanisa. "Basi wewe umfundishaye mwingine, je! hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe?..." (Rum 2:21-24).

UMUHIMU WA KUIOMBEA KWAYA

Ni muhimu kuiombea kwaya bila kukoma. Pasipo Mungu Kwaya haiwezi kufanya hayo tuliyojifunza katika somo hili (Yn 15:5). Kwahiyo basi tuwaombee viongozi wa kwaya, walimu wa kwaya, wapigaji wa vyombo nk. Tukemee roho ya kiburi na mafarakano isipate nafasi katika kwaya. Tuwaombee watunzi wa nyimbo, Bwana awape nyimbo mpya zenye ujumbe mzuri. Tuviombee vyombo vya kwaya visiharibike. Tuwaombee wanakwaya wawe na bidii ya kumtumikia Mungu kwa uimbaji (Rum 12:11).


***********************************************************************************

ASANTE KWA KUSOMA SOMO HILI. TAFADHALI WAELEZE NA WENGINE. UKIWEZA, CHAPA SOMO HILI KWENYE KARATASI, TOA NAKALA NA KUWAGAWIA WANAKWAYA. NA KAZI YAKO HAITAKUWA BURE KATIKA BWANA (1 Kor 15:58). UBARIKIWE!

MAANA YA KUOKOKA!!!!!

Siyo busara kusema kwamba "hakuna kuokoka, haiwezekani kuokoka," huku hatujui hata maana ya kuokoka. Mtu mwenye busara kwa mfano, hawezi kusema hakuna ”Nguvu ya Uvutano“ huku hajui hata maana ya nguvu hiyo.

Watu wengi watajikuta wanakwenda katika mateso ya Jehanam ya moto, kwa sababu tu hawajui maana ya kuokoka, na jinsi ya kuokoka katika mateso hayo. Sasa basi, ni nini maana ya kuokoka?

Kuokoka au kuokolewa, ni kunusurishwa, kuopolewa, kusalimishwa au kuponywa kutoka katika maafa makubwa yaliyo dhahiri kabisa kumpata mtu.

Inaweza ikawa kuponywa kutoka katika hatari ya kifo, adhabu kali au madhara yoyote makubwa yaliyo dhahiri.

Katika hali ya kukosa matumaini ya kukwepa maafa hayo yaliyo dhahiri, inapotokea ghafla njia ya kusalimika; hapo tunasema mtu aliyesalimika au kunusurika, ameokoka. Kwa mfano, mtu asiyejua kuogelea anapotumbukia baharini baada ya mashua aliyokuwa anasafiria kupinduka, halafu akaanza kunywa maji, na kuwa katika hatari ya kufa maji; anapotokea bingwa wa kuogelea, na kumsalimisha mtu wa jinsi hiyo, hapo tunasema kwamba bingwa wa kuogelea, amemuokoa mtu huyo, na mtu huyo ameokolewa au ameokoka.

Miaka kadhaa iliyopita katika nchi yetu ilitokea ajali mbaya ya meli ”Mv Bukoba.“ Meli hiyo ilizama katika Ziwa Victoria ikiwa na abiria; na mamia kwa mamia walikufa maji .Meli hiyo ilipinduka na kuzama, ikiwa chini juu. Mpaka leo, haikuwezekana kuitoa ile meli majini, na hivyo mamia hao ”walizikwa“ katika meli hiyo. Yalikuwa ni maombolezo makubwa ya kitaifa. Ninamfahamu dada mmoja ambaye alikuja kuniona, ili nimwombee kwa Mungu; apate faraja, na kutoka katika hali ya mawazo mengi. Dada huyu alifiwa na ndugu zake 22, kwa mpigo, na wote walizama katika meli hiyo, na hakuna hata mmoja aliyepatikana hata mwili tu wa kuzika. Ndugu hawa wote walijikusanya Dar-Es-Salaam, Dodoma, Tabora na Mwanza na kwenda Bukoba kwenye msiba.

Baada ya msiba, wakaamua wote kwa pamoja kurudi kwa meli hiyo, siku hiyohiyo moja. Matokeo yake, ikawa ni kupata ajali hiyo na kufa maji. Hata hivyo, pamoja na mamia kwa mamia kufa maji katika ajali hiyo mbaya, wako watu wachache ambao walinusurika kufa. Vyombo vya habari vilipokuwa vikitoa taarifa hii, vilisema ”Watu waliookoka katika ajali ya ”Mv Bukoba“, waelezea mkasa uliowapata“. Wale walionusurika katika ajali hiyo, walisemekana wameokoka.

Baada ya kuelewa maana ya neno ”Kuokoka“, hatuna budi kufahamu kwamba, neno ”kuokoka“, linatumika kwa maana hiyohiyo, linapokuwa linahusishwa na ”walokole.“ Labda utaniuliza, ”Kwa vipi walokole wameokoka? Wamenusurika katika mkasa upi?“ Katika kujibu swali hili, unahitajika ufafanuzi wa kina ili tupate kuelewa. Tufuatane sasa hatua kwa hatua, ili upate kuelewa.

Wanadamu wote ni wenye dhambi kutokana na asili yetu. Kutokana na mzazi wetu Adam aliyefanya dhambi, sisi sote tunazaliwa tukiwa na asili ya dhambi na hivyo kujikuta tunatenda dhambi. Kwa mtu mmoja (Adam), dhambi iliingia ulimwenguni na kila mmoja wetu anahesabiwa kuwa na dhambi (Warumi 5:12). Biblia inasema katika Zaburi 51:5, ”Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatiani.“ Sisi sote, tunazaliwa tukiwa na asili ya dhambi. Ndiyo maana utaona mtoto mdogo anasema uongo, ana hasira, wivu n.k. Mtoto mdogo akisikia muziki wa dansi, atakata viuno na kucheza, bila hata kufundishwa. Mtoto mdogo akinyimwa au kucheleweshwa ”nyonyo“ au kunyonya ziwa la mamaye, atakasirika na kumpiga mamaye kofi pamoja na kamkono kake kadogo. Hasira hii imetoka wapi? Ni kutokana na dhambi ya asili ya Adam.

Hivyo kutokana na asili ya dhambi, kila mtu anahesabiwa kuwa ni mwenye dhambi; awe anavuta sigara au havuti sigara. Awe anakunywa pombe au hanywi pombe. Awe anafanya uasherati au hafanyi uasherati. Awe anafanya dhambi hii au nyingineyo, bado kila mwanadamu ni mwenye dhambi. Awe anafanya dhambi nyingi au chache, hiyo haijalishi, bado mwanadamu ni mwenye dhambi kutokana na asili yake. Mnazi unabaki mnazi, ukitoa nazi elfu moja, nazi kumi au usipotoa nazi kabisa. Mnazi, ni mnazi, kutokana na asili yake ya mti. Mwanadamu yeyote, hata akijitahidi kutenda mema, ni kazi bure, bado mbele za Mungu, anahesabiwa kuwa hana haki, ni mkosaji, kutokana na asili yake ya dhambi.Tunasoma katika AYUBU 9:29-31, Nitahukumiwa kuwa ni mkosa; Ya nini nitaabike bure? Ingawaje najiosha kwa maji ya theluji,na kuitakasa mikono yangu kwa sabuni; lakini utanitupa shimoni.“ Tena tunasoma katika ISAYA 64:6, ”Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.“

Sasa basi, matokeo ya dhambi ni nini? Ni adhabu. Hakuna mwenye dhambi atakayekosa adhabu. Lazima kila mwenye dhambi atapata adhabu ya milele yaani kutupwa katika ziwa la moto na kutengwa na Mungu milele (WARUMI 6:23; UFUNUO21:8). Hakuna mtu yeyote mwenye dhambi, yaani asiyekuwa na haki mbele za Mungu atakayeokoka katika adhabu hiyo. Biblia inasema katika ZABURI 119:155, ”Wokovu u mbali na wasio haki“. Kutoa sadaka nyingi, kusali mara tatu au mara tano kwa siku, kuimba kwaya, kipaimara, ubatizo wa utotoni au tendo lolote linaloonekana jema kidini, haliwezi kumfanya mtu anusurike katika adhabu hii ya moto wa milele. Hata kama mtu hanywi pombe, havuti sigara au siyo mwizi, bado tu atakwenda katika moto wa milele kutokana na asili ya dhambi iliypmo ndani yake. Dhambi ya asili ya Adamu, inatosha kabisa kumtupa mtu katika moto wa milele bila nyongeza yoyote ya dhambi.

Wokovu u mbali kabisa na wasio haki, na hakuna mwanadamu mwenye haki mbele za Mungu (AYUBU 25:4). Ili mtu aokoke kutoka katika adhabu ya moto wa milele, lazima kwanza ahesabiwe na Mungu kuwa ni mwenye haki. Biblia inasema katika MITHALI 11:21, ” Hakika mtu mwovu hatakosa adhabu; bali wazao wa wenye haki wataokoka“.

Unaona sasa? Ili mtu anusurike au aokolewe kutoka katika adhabu ya moto wa milele, ni lazima kwanza ahesabiwe haki ya kuingia mbinguni, na Mungu mwenyewe. Mwanadamu anahesabiwa haki namna gani na kuokoka? Hatuhesabiwi haki na Mungu kwa kujitahidi kushika nguzo fulani za dini, kwenda Jumapili Kanisani, kujaribu kuishika sabato, kufanya sakramenti zote au matendo ya sheria. Tunahesabiwa haki kwa imani tu! Kwa imani tu, mtu husafishwa dhambi zake kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani, na Mungu mwenyewe humpa uwezo wa kushinda dhambi, na kumuwezesha kuishi maisha ya utakatifu. Biblia inasema katika WARUMI 3:28, ”Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria“.

Je, mtu anaweza kuokoka akiwa hapa duniani?

Tukijaribu kujitahidi kuacha pombe, sigara au dhambi yoyote, kwa nguvu zetu, hatuwezi! Kwa kujitahidi kwa nguvu za kibinadamu, hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuishi maisha ya utakatifu hapa duniani. Ndiyo maana watu wamekata tamaa na kusema kwamba haiwezekani mtu kuokoka duniani, eti wokovu ni mpaka mbinguni. Je, kuna ukweli katika maneno hayo ? Jibu ni la! Kuokoka ni hapa hapa duniani, siyo mbinguni! Ziko sababu kadha zinazothibitisha kwamba kuokoka ni hapa duniani.



Kwanza, Yesu Kristo alitoka mbinguni na kuja duniani kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Biblia inasema katika LUKA 19:10, ”Kwa kuwa Mwana wa Adam alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.“ Kama wokovu ungekuwa hukohuko mbinguni baada kufa, Yesu asingekuwa na haja ya kuja huku duniani.

Pili, Yesu alipokuwa katika safari zake za injili, akiwa duniani, wakati mmoja aliingia katika nyumba ya mtu mmoja aliyeitwa Zakayo na kumwambia, ”Leo wokovu umefika nyumbani humu.“ (LUKA 19:9). Kama mtu angekuwa anaokoka baada ya kufa, Yesu asingetumia neno, ”Leo“.



Tatu, Neno la Mungu linasema Mungu anapendezwa na watakatifu walioko duniani. Tunasoma katika ZABURI 16:3, ”Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio ninaopendezwa nao“. Neno pia, linasema wazi kwamba tunapaswa kuishi kwa kiasi na utauwa, yaani utakatifu, katika ulimwengu wa sasa (TITO 2:11-12).

Nne, kwa sababu wokovu ni hapa duniani, ndiyo maana Yesu alipokuwa duniani aliwahubiri watu waokoke hapahapa duniani. Kwa maneno yake akihubiri katika YOHANA 5:34, anasema ”Walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.“

Tano, watu waliokuwa duniani walishuhudia kwamba waliokolewa na kuacha dhambi hapahapa duniani. Hawa wanasema katika TITO 3:3-4, Maana hapo zamani, sisi nasi tulikuwa hatuna akili tulikuwa waasi, tumedanganywa huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi (duniani), tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa (kwetu), alituokoa.“ Unaona hapa! Wanatumia maneno, ” Hapo zamani“, na ”Tulikuwa“, wakizungumzia maisha yao ya uovu ya muda uliopita na tena wanatumia neno, ”Alituokoa“, linalozungumzia jinsi walivyookolewa muda fulani uliopita; ingawa bado walikuwa hapahapa duniani.

Kwa nini watu wanasema haiwezekani kuokoka hapa duniani? Kama tulivyogusia kitambo, ni kwa sababu watu wanafikiri kwamba wanaweza kuishi maisha ya utakatifu kwa kujitahidi kwa nguvu zao. Watu waliokata tamaa na kuona kwamba haiwezekani kuishi maisha ya utakatifu hapa duniani, wamejaribu kutumia nguvu za kibinadamu! Jambo hili linaelezwa vizuri katika MATHAYO 19:25-26, ” Wanafunzi waliposikia, walishangaa mno, wakisema Ni nani basi awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali kwa Mungu yote yanawezekana.“ Kwa uwezo wa kibinadamu, hatuwezi kuokoka hapa duniani, lakini kwa uwezo wa Mungu jambo hili ni rahisi sana. Uwezo wa Mungu ulimbadilisha Sauli aliyekuwa mwuaji, na kumfanya Mtume. Sisi nasi kwa imani tu tunapotubu dhambi na kuziacha, tunapata rehema ya kusamehewa dhambi zetu na kupata uwezo wa kushinda dhambi duniani aliokuwa nao Yesu Kristo (MITHALI 28:13; WAEBRANIA 4:14-16).

Ni muhimu kufahamu kwamba mtu yeyote akimwendea Yesu, kwa imani, na kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kuziacha, atasamehewa dhambi zake mara moja maana neno lake linasema katika YOHANA 6:37, ”… wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.“ Hata kama dhambi zetu ni nyingi kiasi gani, Yeye hutusamehe mara moja (ISAYA 1:18). Siyo hilo tu, nimuhimu kufahamu kwamba msamaha huu wa dhambi huambatana na wokovu! Biblia inasema katika LUKA 1:17, ”Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao.“ Ukisamehewa dhambi zako, kwa ghafla tu, utaona kiu yote ya dhambi imehama kabisa na unapenda tu kufanya mapenzi ya Mungu, huku ukiwa na uwezo wa kushinda dhambi. Je, unapenda kuokoka leo? Najua unapenda. Basi, kwa imani fuatisha sala hii,

"Mungu Baba, ninashukuru kwa ujumbe huu. Ninatubu dhambi zangu kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo naomba unisamehe dhambi zangu zote za kuzaliwa na kutenda. Nisafishe dhambi zote kwa damu yako iliyomwagika msalabani na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa. Asante kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu. Amen.“

Tayari sasa umeokoka. Ili uzidi kuukulia wokovu ulioupokea leo, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI!!!

Wednesday, March 3, 2010

WHAT NEXT AFTER DEATH!!!!!

Way 2 Groovy Site
Where will you go after you die?









Home
Where will you spend eternity?
True Grace
Cries from the unborn
Food for thought
Favorite Musicians




1. Acknowledge you are a sinner:
"For all have sinned, and come short of the glory of God;'' Romans 3:23.

Yes, you too have fallen short of Heaven because of your sin. You may be better than many others. but compared to Jesus "They are all gone out of the way, they are together become unprofitable; there is none that doeth good, no, not one." Romans 3:12.

2. Realize and acknowledge:

" For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord".
Romans 6:23

There are two kinds of death, physical and spiritual. One we inherited from Adam and the other we earn for ourselves. Adam's sin brought physical death totally. But, because of our sin. we must die a second death eternally in Hell, unless we find a way to pay for our sin and thereby remove its penalty of Fire and brimstone, which is the second death.

"But the fearful, and unbelieving, and abominable, and murderers, and whoremongers, and sorcerers, and idolaters, and all liars, shall have their part in the lake which burneth with fire and brimstone: which is the second death." Revelation 21: 8.

3. Realize and acknowledge:

"For I delivered unto you first of all that which I also received, how that Christ died for our sins according to the scriptures;"

I Corinthians 15:3.

Jesus paid the entire price for you by his death on the cross. A Holy and just God set the price on sin, and then in love, paid it Himself in the person of Christ.

4. Realize and acknowledge:

'the gift of God is eternal life through Jesus Christ," Romans 6:23.

He bought it. He owns it. He freely gives it. We are not saved by believing a story about a has-been. Christ is alive today! "knowing that Christ being raised from the dead dieth no more, death hath no more dominion over him," Romans 6:9.

He has power and victory over death and sin and offers the same to you as a gift, not a reward.

5. Realize and acknowledge:

"Whosoever shall call upon the name of the Lord shall be saved,'' Romans 10:13.

This is a promise. Whosoever means you.

Not whosoever is a church member, or is baptized, or is confirmed, or takes communion, or does the best he can, but whosoever shall call believing in Jesus.

Here is how you can be 100 per cent sure of Heaven.

6. Confess and ask:

Just say this simple prayer,

Dear Lord,

I'm sorry I am a sinner, please forgive of my sins and come into my heart.

In Jesus Name,

Amen

After you say the prayer if you really meant it. Jesus will never leave you. Your sins are forgiven. You are saved forever.

" Let your conversation be without covetousness; and be content with such things as ye have: for he hath said, I will never leave thee, nor forsake thee." Hebrews 13:5.

" And I give unto them eternal life; and they shall never perish, neither shall any man pluck them out of my hand.
My Father, which gave them me, is greater than all; and no man is able to pluck them out of my Father's hand.
I and my Father are one." John 10:28-30.

"Who shall separate us from the love of Christ? shall tribulation, or distress, or persecution, or famine, or nakedness, or peril, or sword?
As it is written, For thy sake we are killed all the day long; we are accounted as sheep for the slaughter.
Nay, in all these things we are more than conquerors through him that loved us.
For I am persuaded, that neither death, nor life, nor angels, nor principalities, nor powers, nor things present, nor things to come,
Nor height, nor depth, nor any other creature, shall be able to separate us from the love of God, which is in Christ Jesus our Lord." Romans 8:35-39

Nothing can separate us from Jesus if you meant what you said when you prayed the above prayer, then you are His child forever.










I would really love to know if you asked Jesus into you heart or if you have any further question about salvation.

email me